Alhamisi, 1 Oktoba 2015

AJALI

Mtoto wa Marehemu Paul Walker kapeleka Kesi ya Kifo cha baba yake Mahakamani, madai yake ni haya…

By
Atkin mulenga 
on
Marehemu Paul Walker alikuwa mmoja ya wakali ambao wamecheza movie za Fast & Furious… Kifo chake ni moja kati ya vifo vilivyoshtua na kuwaumiza watu wengi Duniani.
Jamaa alifariki kwa ajali ya gari aina ya Porsche Carrera GT ambayo ilikuwa inaendeshwa na rafiki yake, Roger Rodas na Paul mwenyewe alikuwa amekaa upande wa pili.. hiyo ilikuwa November 30 2013, California Marekani.
Herculesstreet
Hili ndio eneo ambalo Paul Walker alipata ajali.
Leo kuna story ambayo imepewa uzito sana mitandaoni, inahusu ishu ya mtoto wa kike wa Paul Walker ambaye anaitwa Meadow Rain Walker mwenye umri wa miaka 16… amefungua mashtaka kuishtaki Kampuni ya Porsche kwamba ajali iliyopelekea kifo cha baba yake miaka miwili iliyopita, ilitokana na gari kuwa na matatizo na anadai kwamba muundo wa gari hiyo haikuwa gari ya kutembelea, ila ilikuwa na muundo wa gari ya mashindano.
Kingine ambacho kiko kwenye Mashtaka hayo ni kwamba wanadai gari hiyo haikuwa na mfumo mzuri wa umeme, kwa hiyo ilikuwa ni ngumu pia kwa Paul pamoja na mshkaji wake kutoka salama baada ya kupata ajali hiyo… Uchunguzi wa Maofisa Usalama wa Los Angeles ulitoa Ripoti yao kwamba sababu ya ajali hiyo ilikuwa mwendokasi.
Paul alifariki wakati ambao walikuwa kwenye maandalizi ya Movie ya Fast & Furious 7
Paul alifariki wakati ambao walikuwa kwenye maandalizi ya Movie ya Fast & Furious 7
Kwenye Ripoti hiyo pia Wanausalama wanasema Marehemu wote wawili hawakuwa wametumia kilevi cha aina yoyote na wala hawakutumia dawa za Kulevya.
Wimbo ambao uliandaliwa kama Dedication kwa Paul Walker ni huu hapa.. Wiz KhalifaFeat. Charlie Puth– ‘See You Ag


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni