Ijumaa, 1 Mei 2015

January Makamba - Tanzania Mpya

Mashabiki wa AC Milan waja na staili mpya ya kukaa uwanjani… unajua kwa sababu gani?

fans ac
Kutofanya vizuri kwa klabu ya AC Milan kumewafanya mashabiki wa kukasirishwa.. hii sio klabu ya kwanza kukutwa na noma ya namna hii toka kwa mashabiki.. Arsene Wengerni moja ya makocha ambao wamepitia sana vipindi vigumu vya kukataliwa na mashabiki wa Klabu ya Arsenal, safari hii balaa limehamia AC Milan.
Wenger-despair-main
Mmiliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi ambaye ameiongoza klabu hiyo kwa miaka zaidi ya 30 ameonekana kuchokwa na mashabiki wa timu hiyo ambao sasa wameamua kufanya kama mgomo hivi.. wanataka mmiliki abadilishwe kwa kuwa timu haijafanya vizuri kwenye matokeo ya mechi zake nyingi walizocheza.
basta
Mashabiki hao wamekaa uwanjani kwa mtindo ambao unasomeka ‘BASTA‘ ambao tafsiri yake ni “sasa imetosha”.
Wengi wanataka kiongozi huyo aiuze klabu yake ili mtu mwingine inunue ifanye vizuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni