Ijumaa, 1 Mei 2015

Picha za Wema na gauni la harusi, pete ya ndoa @Instagram, eti ni ndoa ya ukweli?? Iko kwa Soudy Brown..

WSepetu
Pichaz ziko mitandaoni.. Wema Sepetu nae kapost kwenye ukurasa wake wa Instagram, amevaa gauni la harusi.. Wema Sepetu ameolewa kweli au movie????
Soudy Brown kamtafuta Wema.. alichokijibu ni kwamba ni kweli ameolewa ila hayuko tayari kumtaja mume wake.. amesema kuwa kaamua kufunga ndoa ya siri kwa kuogopa kupigwa ‘juju’.
Sepetuur
Wema amesema ndoa yao ilifungwa bomani kwa sababu mume wake ni mkristo.. kingine ni kwamba harusi ilihudhuriwa na watu watano pamoja na familia yake ila mwishoni mwa mwezi huu watafanya sherehe rasmi.
Kuhusu ishu ya kutopata mtoto Wema amesema mwanaume huyo anajua na amekubaliana na hiyo hali lakini inawezekana kwake wakapata mtoto.

Alikozaliwa Vanessa Mdee, watoto? mume? kipya alichosema kuhusu Jux? vyote viko hapa

Mtanzania aliyepata bahati ya kwenda marekani na Akon kupitia shindano la trace music star..

Diamond Platnumz alipokasirika na kuuonyesha upande mwingine wa nyumba yake, hii ni ya chumbani kwake

Diamond Zari 1
Kwenye hii post aliandika ‘State House tym Hii..😊
Super star kutokea Tanzania Diamond Platnumz usiku wa April 29 2015 aliamua kuonyesha upande mwingine wa nyumba yake aliyoijenga Dar es salaam ambapo alipost post zaidi ya moja kwa kile kinachoonekana kuwa ni baada ya kukasirishwa na comment ya follower wake Instagram.
Post iliyofata baada ya hii aliandika ‘Crazy Us 😄…Tafta kopo Ujiandae Kutapika maana Ndimu Zishakuzoea….😁😂 #StateHouseByNight
Unaweza kutazama hizi video fupi hapa chini uone alichoonyesha.

Post iliyofata pia alionyesha chumba chake tena na mrembo Zari akiwa kitandani na kuandika ‘Sasa si uniunfollow kama Nakukera👀.. hupendi halaf bado Umeng’ang’ania tu Kwenye Page yangu….Utaja kufa kwa Hasira bure’      
Post ya mwisho aliyoiweka ni hii hapa chini aliyoambatanisha na maneno yake ‘Nimemuuliza “unanita” kasema Ndio!… nije? kasema “Njoo”… siju niiweke inayofata au??? ‘
Diamond na mpenzi wake Zari the boss lady wataenjoy na Watanzania kwenye#ZariAllWhiteParty Mlimani City Dar es salaam ambapo mastaa kibao watakuwepo akiwemo rapper A.K.A wa South Africa na Shetta.
Diamond na Zari

January Makamba - Tanzania Mpya

Mashabiki wa AC Milan waja na staili mpya ya kukaa uwanjani… unajua kwa sababu gani?

fans ac
Kutofanya vizuri kwa klabu ya AC Milan kumewafanya mashabiki wa kukasirishwa.. hii sio klabu ya kwanza kukutwa na noma ya namna hii toka kwa mashabiki.. Arsene Wengerni moja ya makocha ambao wamepitia sana vipindi vigumu vya kukataliwa na mashabiki wa Klabu ya Arsenal, safari hii balaa limehamia AC Milan.
Wenger-despair-main
Mmiliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi ambaye ameiongoza klabu hiyo kwa miaka zaidi ya 30 ameonekana kuchokwa na mashabiki wa timu hiyo ambao sasa wameamua kufanya kama mgomo hivi.. wanataka mmiliki abadilishwe kwa kuwa timu haijafanya vizuri kwenye matokeo ya mechi zake nyingi walizocheza.
basta
Mashabiki hao wamekaa uwanjani kwa mtindo ambao unasomeka ‘BASTA‘ ambao tafsiri yake ni “sasa imetosha”.
Wengi wanataka kiongozi huyo aiuze klabu yake ili mtu mwingine inunue ifanye vizuri.